Masharti ya Mkataba wa kulima Uyoga

Uyoga Company LogoUYOGA COMPANY LTD
44R, ITEGA. S.L.P 608, DODOMA
Registration No. 97761 TIN 121-112-477
Web: http://www.mushroomuyoga.co.tz,
Mail: sales@mushroomuyoga.co.tz
TOLL FREE No. 0800711711
Branch office: 28R, Mkapa road, P.O. Box 6, Bagamoyo

1. UTANGULIZI
Kampuni ya Uyoga Company Ltd yenye makao makuu mjini Dodoma ina lengo la kununua tunda la Uyoga toka kwa Wakulima. Kampuni itakuwa inazalisha mbegu na kuwauzia wakulima kwa msimu wa kwanza na kuwapatia bure kwa misimu mingine. Ili kufanikisha lengo hili kampuni itaingia mkataba na wakulima wa zao na kuwapa maelekezo kwa njia ya simu, picha, video (WhatsApp), kupitia mtandao wa kampuni (www.mushroomuyoga.co.tz) na ikibidi mtaalamu wa kampuni ataenda kwenye shamba la Mkulima.

2. MAJUKUMU YA MKULIMA
Yafuatayo ni majukumu ya Mkulima:-

(a) Mkulima atalazimika kununua mbegu baada ya kusaini mkataba, na kupata maelekezo ya kukadiliwa kiasi cha mbegu kutoka kwa mtaalamu wa Kampuni. Bei ya mbegu kwa chupa ya 240ml ni TZS 3,000/-. Kiasi cha chini cha kununua ni chupa 100 (sawa na TZS 300,000/-) ambazo zitatumika kupanda mifuko 1000 ambayo inaingia kwenye banda sawa na vyumba viwili vya 3mx3m. Mkulima atauza tunda la Uyoga kwa kampuni kwa bei ya TZS 4,000 kwa kilo ya uyoga mbichi (Chaza, Kifungo na Chamizi) au mkavu wa kuvunjika kama njiti ya kibiriti kwa TZS 15,000 kwa kilo.

(b) Mkulima atalipa malipo ya mbegu kupitia benki zifuatazo:-

(i) NMB A/C. 21003500141, Jina: TUVAE LTD, au
(ii) AZANIA BANK LTD, A/C.005005143608270001, Jina UYOGA Co. LTD
(iii) CRDB, A/C. 0112003544000, Jina Hussein Mzara
(iv) BARCLAYS, AC. 0162005103, Jina Hussein Mzara

(c) Mkulima atalima uyoga kwa taratibu sahihi za kitaalamu.

(d) Mkulima atapokea mbegu za uyoga toka Uyoga Company na atazitumia kwenye shamba lake tu.

(e) Mkulima atagharamia ujenzi wa banda lake, vimeng’enywa, uchemshaji pamoja na kupanda mbegu.

(f) Mkulima ampe ruksa Wakala wa kampuni kuingia bandani na kukagua maendeleo ya uyoga muda wowote pasipo kuwa na kikwazo.
(g) Mkulima atakuwa anatoa taarifa ya mavuno ya uyoga kila avunapo kwa njia ya simu, Whatsaap au kupiga simu.
(h) Mkulima atakuwa anasaini karatasi ya Wakala pale tu atembelewapo.
(i) Mkulima atauza mazao yake yote ya uyoga kwa UYOGA COMPANY kwa bei iliyo oneshwa kwenye kifungu Na.2 (a) hapo juu.

3. MAJUKUMU YA MNUNUZI
Yafuatayo ni majukumu ya Mnunuzi:-
(a) Kumpatia Mkulima mbegu kwa mahitaji ya kupanda kwa muda husika.
(b) Kuchukua uyoga uliovunwa aidha mbichi au mkavu.
(c) Kumlipa Mkulima gharama za uyoga uliovunwa kwa mwezi mzima kabla ya tarehe 15 ya mwezi unaofuata.

4. UTARATIBU WA MALIPO
(a) Mkulia atawekewa malipo kwenye akaunt yake ya benki au kupatiwa hundi kwa malipo yanayozidi TZS 100,000/-
(b) Kwa malipo yasiyo zidi TZS 100,000/- atalipwa kupitia simu yake.

5. KUSITISHWA KWA MKATABA
(a) Mkataba huu ni wa mwaka mmoja toka tarehe ya leo; hivyo basi mara baada ya
kumalizika kwa muda wa mkataba ni hiari ya pande zote mbili aidha kusitisha au
kuingia katika mkataba upya.
(b) Mkataba utasitishwa pale tu aidha mmoja wa mshika mkataba huu atakaposhindwa kutimiza majukumu yake.

6. SABABU ZA KUSITISHWA KWA MKATABA

Zifuatazo ni sababu za kusitishwa kwa mkataba:-
(a) Mnunuzi anaposhindwa kumlipa Mkulima kwa wakati.
(b) Mkulima atakapo tumia mbegu ambazo hazijatoka Uyoga Company.
(c) Itakapo bainika kwamba Mkulima anatumia mbolea za kiwandani kwenye vimeng’enywa vyake.
(d) Umwagiliaji/uloweshaji wa uyoga siku ya kuvuna.
(e) Kutokuweka dawa ya detto kwenye kibwawa cha mlango wa kuingilia bandani.
(f) Uzembe wa Mkulima utakao sababishwa mazao kuto kuota.
(g) Ukiukwaji wa kipengele chochote kwenye mkataba huu.

7. KATAZO
(a) Si ruhusa kwa mkulima au mtu yeyote anayefanya kazi kwa niaba ya Mkulima au aliye karibu na mkulima yeyote katika mkataba huu kujishughulisha na biashara ya mazao yatokanayo na uyoga, kutumia ujuzi, nembo, maandishi, viambatanishi, virutubishi ama vifungashio vya kampuni ama vinavyo fanana na kampuni ambaye kwa mkataba huu anajulikana kama mnunuzi.
(b) Kwamba Mkulima yeyote atakaye bainika kukiuka kipngele 7(a) hatua kali dhidi yake zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kulipa fidia na kufikishwa katika mahakama husika.

8. KUTATUA MGOGORO
Endapo kutakuwa na tatizo lolote kuhusiana na mkataba huu au mgogoro wowote baina ya mkulima na mnunuzi katika mahakama husika na sheria za mikataba na sheria zingine zinazo ambatana na mkataba husika zitatumika kutatua tatizo hilo.

9. APIZO
Mimi kama Mkulima wa zao la Uyoga wa kabila ya Chaza (Oyster mushroom/ Pleurotus Spp.), Chamizi (Ganoderma Lucidum) na Kifungo (Agaricus Bisporus) nimekubaliana na
maelezo yote ya hapo juu.

A Farmer has to fill the below form (Mkulima ajaze fomu hii)

Jina la kwanza na la pili

Barua Pepe

Mahali unapoishi

Mahali ambapo shamba litalimwa

Namba ya simu ya mawasiliano

Namba ya simu ya malipo

Jina la Benki la kupokelea pesa

Namba ya akaunti ya Benki