Masharti ya Mkataba wa kulima Uyoga

Uyoga Company LogoUYOGA COMPANY LTD
44R, ITEGA. S.L.P 608, DODOMA
Registration No. 97761 TIN 121-112-477
Web: http://www.mushroomuyoga.co.tz,
Mail: sales@mushroomuyoga.co.tz
TOLL FREE No. 0800711711
Branch office: 28R, Mkapa road, P.O. BOX 6, Bagamoyo

1. UTANGULIZI
Kampuni ya Uyoga Company Ltd yenye makao makuu mjini Dodoma ina lengo la kununua tunda la Uyoga toka kwa Wakulima. Kampuni itakuwa inazalisha mbegu na kuwauzia wakulima kwa msimu wa kwanza na kuwapatia bure kwa misimu mingine. Ili kufanikisha lengo hili kampuni itaingia mkataba na wakulima wa zao na kuwapa maelekezo kwa njia ya simu, picha, video (WhatsApp), kupitia mtandao wa kampuni (www.mushroomuyoga.co.tz) na ikibidi mtaalamu wa kampuni ataenda kwenye shamba la Mkulima.

2. MAJUKUMU YA MKULIMA
Yafuatayo ni majukumu ya Mkulima:-
(a) Mkulima atalazimika kununua mbegu baada ya kusaini mkataba, na kupata maelekezo ya kukadiliwa kiasi cha mbegu kutoka kwa mtaalamu wa Kampuni. Bei ya mbegu kwa chupa ya 240ml ni TZS 3,000/-. Kiasi cha chini cha kununua ni chupa 100 (sawa na TZS 300,000/-) ambazo zitatumika kupanda mifuko 1000 ambayo inaingia kwenye banda sawa na vyumba viwili vya 3mx3m. Mavuno ya uyoga mbichi kwa miezi mitatu yanatakiwa yawe 1000Kg. Mkulima atauza tunda la Uyoga kwa kampuni kwa bei ya TZS 4,000 kwa kilo ya uyoga mbichi (Chaza, Kifungo na Chamizi) au mkavu wa kuvunjika kama njiti ya kibiriti kwa TZS 15,000 kwa kilo.
(b) Mkulima atalipa malipo ya mbegu kupitia benki zifuatazo:-
(i) AZANIA BANK LTD, A/C.005005143608270001, Jina UYOGA Co. LTD
(ii) NMB BANK A/C. 21003500141, Jina: TUVAE LTD, au
(iii) I &M BANK A/C 010009521101, Jina TUVAE LTD, au
(iv) CRDB, A/C. 0112003544000, Jina Hussein Mzarazila Rajabu
(v) BARCLAYS, AC. 0162005103, Jina Hussein Mzarazila Rajabu
(c) Mkulima atalima uyoga kwa taratibu sahihi za kitaalamu.
(d) Mkulima atapokea mbegu za uyoga toka Uyoga Company na atazitumia kwenye shamba lake tu.
(e) Mkulima atagharamia ujenzi wa banda lake, vimeng’enywa, uchemshaji
pamoja na kupanda mbegu.
(f) Mkulima ampe ruksa Wakala wa kampuni kuingia bandani na kukagua
maendeleo ya uyoga muda wowote pasipo kuwa na kikwazo.
(g) Mkulima atakuwa anatoa taarifa ya mavuno ya uyoga kila avunapo kwa njia
ya simu, Whatsaap au kupiga simu.
(h) Mkulima atakuwa anasaini karatasi ya Wakala pale tu atembelewapo.
(i) Mkulima atauza mazao yake yote ya uyoga kwa UYOGA COMPANY kwa bei
iliyo oneshwa kwenye kifungu Na.2 (a) hapo juu.

3. MAJUKUMU YA MNUNUZI
Yafuatayo ni majukumu ya Mnunuzi:-
(a) Kumpatia Mkulima mbegu kwa mahitaji ya kupanda kwa muda husika.
(b) Kuchukua uyoga uliovunwa aidha mbichi au mkavu.
(c) Kumlipa Mkulima gharama za uyoga uliovunwa kwa mwezi mzima kabla ya tarehe
15 ya mwezi unaofuata.

4. UTARATIBU WA MALIPO
(a) Mkulia atawekewa malipo kwenye akaunt yake ya benki au kupatiwa hundi kwa malipo
yanayozidi TZS 100,000/-
(b) Kwa malipo yasiyo zidi TZS 100,000/- atalipwa kupitia simu yake.

5. KUSITISHWA KWA MKATABA
(a) Mkataba huu ni wa mwaka mmoja toka tarehe ya leo; hivyo basi mara baada ya
kumalizika kwa muda wa mkataba ni hiari ya pande zote mbili aidha kusitisha au kuingia
katika mkataba upya.
(b) Mkataba utasitishwa pale tu aidha mmoja wa mshika mkataba huu atakaposhindwa
kutimiza majukumu yake.
6. SABABU ZA KUSITISHWA KWA MKATABA
Zifuatazo ni sababu za kusitishwa kwa mkataba:-
(a) Mnunuzi anaposhindwa kumlipa Mkulima kwa wakati.
(b) Mkulima atakapo tumia mbegu ambazo hazijatoka Uyoga Company.
(c) Itakapo bainika kwamba Mkulima anatumia mbolea za kiwandani kwenye vimeng’enywa vyake.
(d) Umwagiliaji/uloweshaji wa uyoga siku ya kuvuna.
(e) Kutokuweka dawa ya detto kwenye kibwawa cha mlango wa kuingilia bandani.
(f) Uzembe wa Mkulima utakao sababishwa mazao kuto kuota.
(g) Ukiukwaji wa kipengele chochote kwenye mkataba huu.

7. KATAZO
(a) Si ruhusa kwa mkulima au mtu yeyote anayefanya kazi kwa niaba ya Mkulima au aliye
karibu na mkulima yeyote katika mkataba huu kujishughulisha na biashara ya mazao
yatokanayo na uyoga, kutumia ujuzi, nembo, maandishi, viambatanishi, virutubishi ama
vifungashio vya kampuni ama vinavyo fanana na kampuni ambaye kwa mkataba huu
anajulikana kama mnunuzi.
(b) Kwamba Mkulima yeyote atakaye bainika kukiuka kipngele 7(a) hatua kali dhidi yake
zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kulipa fidia na kufikishwa katika mahakama husika.

8. KUTATUA MGOGORO
Endapo kutakuwa na tatizo lolote kuhusiana na mkataba huu au mgogoro wowote baina ya
mkulima na mnunuzi katika mahakama husika na sheria za mikataba na sheria zingine
zinazo ambatana na mkataba husika zitatumika kutatua tatizo hilo.

9. APIZO
Mimi kama Mkulima wa zao la Uyoga wa kabila ya Chaza (Oyster mushroom/ Pleurotus
Spp.), Chamizi (Ganoderma Lucidum) na Kifungo (Agaricus Bisporus) nimekubaliana na
maelezo yote ya hapo juu.